Rabat, Morocco
Mshambuliaji nyota wa Yanga, Clement Mzize ametwaa tuzo ya bao bora la mwaka 2025, tuzo iliyotolewa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) Jumatano hii Novemba 19, 2025.
Tuzo hiyo ilitolewa katika hafla maalum iliyofanyika mjini Rabat na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa soka ndani na nje ya bara ya Afrika.
Mzize alifunga bao hilo katika mechi ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Yanga na TP Mazembe iliyochezwa Januari mwaka huu kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam na Yanga kutoka na ushindi wa mabao 3-1.
Katika kipengele cha bao bora, Mzize alikuwa akichuana na Ghizlane Chebbak, Abdellah Ouazane, Barbra Banda, Anas Roshdy, Asharaf Tapsoba, Calvin Fely, Ibrahim Adel, Jean Claude, Ndabayithethwa Ndlonolo, Refiloe Jane, Oussama Lamlioui na Soufiane Bayazid.
Hii ni mara ya pili kwa timu ya Tanzania kutoa mshindi wa tuzo hiyo, hapo kabla mchezaji nyota aliyekuwa Simba, Pape Sakho aliwahi kubeba tuzo hiyo takriban miaka mitatu iliyopita.
Ushindi wa Mzize umekuja wakati mchezaji huyo akiwa majeruhi na katika siku za hivi karibuni amekuwa akihusishwa na mipango ya kuihama Yanga, mipango ambayo hata hivyo haikuwahi kufanikiwa.
Kimataifa Mzize abeba tuzo bao bora CAF
Mzize abeba tuzo bao bora CAF
Read also
