Berlin, Ujerumani
Bao la kichwa la Harry Kane alilofunga dakika za nyongeza limeiokoa Bayern Munich na hatimaye kutoka sare ya 2-2 dhidi ya Union Berlin katika mechi ya Ligi Kuu Ujerumani ‘Bundesliga’ iliyopigwa Jumamosi hii.
Kane alifunga bao hilo katika dakika ya nne kwenye dakika za nyongeza na hivyo kuiwezesha Bayern kutoka uwanjani na pointi katika mechi ambayo vinara hao wa Bundesliga walipambana kusaka bao la kusawazisha.
Kwa Kane hilo linakuwa bao lake la 23 msimu huu kwa michuano yote na linabaki kuwa bao ambalo limewaokoa vinara hao wa Bundesliga kupoteza mchezo.
Union Berlin ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya 27 ya mchezo huo, bao lililofungwa na Danihlo Doekhi kwa shuti lililotokana na mpira wa kona.
Bayern walisawazisha katika dakika ya 39 mfungaji akiwa ni Luis Diaz aliyeitumia vyema pasi ya Josip Stanisic lakini Doekhi tena akaongeza bao la pili katika dakika ya 83, bao lililotokana na mpira wa adhabu.
Bao hilo liliwapa wenyeji Union Berlin matumaini ya kutoka uwanjani na pointi tatu lakini Kane alifuta matumaini hayo kwa bao la kichwa lililotokana na krosi ya Tom Bischof, bao lililofanya ubao usomeke 2-2.
Kimataifa Kane aokoa jahazi Bayern
Kane aokoa jahazi Bayern
Read also
