Na mwandishi wetu
Yanga imepangwa Kundi B katika Ligi ya Mabingwa Afrika, kundi linalotajwa kuwa gumu na hivyo kuibua hofu juu ya nafasi ya timu hiyo kufanya vizuri na kusonga mbele katika.
Katika kundi hilo Yanga imepangwa na timu za Al Ahly ya Misri, JS Kablie ya Algeria na AS FAR ya Morocco, timu ambazo zote zinatajwa kuwa tishio katika soka la Afrika.
Timu zinazotajwa zaidi kuiweka Yanga pagumu ni AS FAR ya Morocco na Al Ahly ya Misri, ubora wa timu hizi katika soka la Afrika ni jambo lililo wazi ingawa pia JS Kablie si timu ya kupuuzwa hata kidogo.
Ukiachana na hofu ya Yanga kusonga mbele ambayo ni hofu iliyopo Tanzania, kundi jingine linalojadiliwa zaidi kote Afrika ni Kundi A linalowakutanisha mabingwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa Afrika, RS Berkane ya Morocco na mabingwa watetezi wa Kombe la Shirikisho Afrika FC Pyramids ya Misri.
Michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kama ilivyo kwa ile ya Kombe la Shirikisho Afrika hushirikisha klabu bingwa za soka barani Afrika na husimamiwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF).
Makundi ya timu za Ligi ya Mabingwa Afrika ni kama ifuatavyo…
Kundi A: RS Berkane (Morocco), Pyramids FC (Misri), Rivers United (Nigeria), Power Dynamos (Zambia)
Kundi B: Al Ahly (Misri), Yanga (Tanzania), AS FAR (Morocco), JS Kabylie (Algeria)
Kundi C: Mamelodi Sundowns (Afrika Kusini), Al Hilal (Sudan), MC Alger (Algeria), St Éloi Lupopo (DR Congo)
Kudni D: Espérance de Tunis (Tunisia), Simba SC (Tanzania), Petro de Luanda (Angola), Stade Malien (Mali)
Makundi ya timu za Kombe la Shirikisho Afrika ni kama ifuatavyo…
Kundi A: USM Alger (Algeria), Djoliba AC (Mali), Olympique de Safi (Morocco), FC San Pedro (Ivory Coast)
Kundi B: Wydad Casablanca (Morocco), AS Maniema (DR Congo), Azam FC (Tanzania), Nairobi United (Kenya)
Kundi C: CR Belouizdad (Algeria), Stellenbosch FC (Afrika Kusini), AS Otoho (Congo), Singida Black Stars (Tanzania)
Kundi D: Zamalek (Misri), Al Masry (Misri), Kaizer Chiefs (Afrika Kusini), ZESCO United (Zambia)
Kimataifa Kundi la Yanga ligi ya mabingwa lazua hofu
Kundi la Yanga ligi ya mabingwa lazua hofu
Read also
