New York, Marekani
Wanadada ndugu waliojipatia umaarufu duniani kupitia mchezo wa tenisi, Venus na Serena Williams wamejipanga katika kuhakikisha wanatoa fursa kwa watoto wanaopitia mazingira magumu.
Venus na mdogo wake Serena katika kutekeleza mkakati huo kupitia Williams Family Excellence Program watakuwa wakitumia umaarufu wao kwenye tenisi kutoa msaada wa elimu katika jamii zenye matatizo mbalimbali.
Mpango huo ulitangazwa rasmi hivi karibuni wakati wa michuano ya tenisi ya US Open kwa mechi za wanawake zikiwa hatua ya nusu fainali ambapo Venus alishiriki katika halfa iliyofanyika uwanjani.
Katika mpango huo walengwa watakuwa wanafunzi waliomaliza masomo ya sekondari kwa kuendeleza vipaji vyao lengo likiwa kuwafikia wahitaji zaidi ya 2,500 wenye umri kati ya miaka 13 hadi 25.
Mpango huo wa kila mwaka utafikia ukomo mwaka 2035 ambapo kwa kipindi chote taasisi ya USTA itakuwa na jukumu la kuwasaka vijana wenye vipaji vikiwamo vya michezo wanaotoka jamii zenye uwezo mdogo na ambao wana uhitaji wa kifedha.
Vijana hao watasaidiwa kupata mafunzo ya kuendeleza vipaji vyao katika vyuo na taasisi za mafunzo kwa gharama nafuu au bila gharama na baadaye kuwekwa katika makambi na kushirikishwa katika mashindano mbalimbali.
Serena na Venus ni majina maarufu duniani kwenye mchezo wa tenisi wakiwa na tuzo mbalimbali walizobeba baada ya kuibuka washindi katika mashindano makubwa ya kimataifa yakiwamo ya US Open, Australia, Paris na mengineyo.
Sports Mix Serena, Venus kusaidia wenye uhitaji
Serena, Venus kusaidia wenye uhitaji
Read also
