Na mwandishi wetu
Timu ya Simba hatimaye imefuzu hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika na hivyo kuzifanya timu za Tanzania zilizofuzu hatua hiyo kwenye michuano inayoandaliwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kufikia nne.
Simba imefikia hatua hiyo leo Jumapili Oktoba 26, 2025 baada ya kutoka sare ya bila kufungana na Nsingizini Hotspur ya Eswatini katika mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.
Matokeo hayo yanaifanya Simba kuwa imefuzu kwa ushindi wa jumla wa mabao 3-0, matokeo ambayo waliyapata katika mechi ya awali iliyochezwa mwishoni mwa wikiendi iliyopita ambapo Simba walikuwa ugenini.
Simba sasa inaungana na mahasimu wao Yanga ambao pia wamefuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa wakati Azam FC na Singida Big Stars zimefuzu hatua kama hiyo kwenye Kombe la Shirikisho Afrika.
Timu zote hizo sasa zinasubiri hadi Novemba 3 mwaka huu ili kuwajua wapinzani wao katika droo ya kupanga makundi ya timu zilzofikia hatua hiyo.
Wakati huo huo Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, kupitia kwa katibu mkuu wa wizara hiyo, imezipongeza timu zote nne zilizofikia hatua hiyo.
Kimataifa Simba yazifuata Yanga, Azam makundi Afrika
Simba yazifuata Yanga, Azam makundi Afrika
Read also
