London, England
Wakati Arsenal ikisubiri kuivaa Atletico Madrid kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, kocha wa Arsenal, Mikel Arteta amemsifia kocha wa Atletico, Diego Simeone (pichani) akidai anaamini kocha huyo anaweza kuchukua nafasi ya kocha yeyote England.
Simeone amekuwa kocha wa Atletico tangu Desemba 2011 akiwa sasa anafikisha miaka 14 na timu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu Hispania maarufu La Liga.
Hakuna kocha wa timu ya Ligi Kuu England (EPL) aliyedumu kwa kipindi kirefu na timu yake kama ilivyo kwa Simeone, kwa England kocha anayeongoza kwa kuwa muda mrefu kwenye timu moja ni Pep Guardiola aliyejiunga na Man City mwaka 2016.
Aneyeshika nafasi ya pili baada ya Pep kwa kudumu muda mrefu na timu moja ni Arteta ambaye alijiunga na Arsenal mwaka 2019 na hadi sasa yuko na timu hiyo.
Arteta alikuwa akijibu swali la waandishi wa habari baada ya kuulizwa kama kuna kitu kinamhamasisha kwa Simeone kutokana na muda ambao amekaa akiwa na Atletico.
“Ni kweli yupo Simeone ambaye namuangalia na kujifunza kutoka kwake katika mazingira mengi na kinachonigusa zaidi ni hamasa aliyonayo,” alisema Arteta kabla ya mechi hiyo.
“Nafikiri kwa kipindi ambacho amekuwa katika soka na katika timu hiyo hiyo na wachezaji hao hao na hapo unajiuliza unakuwaje na mkono na nguvu ya kubadilika na kuwa na utayari wa kupata ushindi,” aliongeza Arteta.
Arteta alisema kwamba makocha wanaishi katika mazingira magumu na kitendo cha kuwaza kuwashawishi wachezaji unatakiwa pia kuwa mtu wa kipekee.
“Simjui yeye (Simeone) binafs lakini kila kitu ninachokisikiti kuhusu yeye ni kwamba yuko vizuri mno katika kazi yake na hiyo ndiyo sababu hasa ya kumfanya adumu katika kiwango hicho,” alisema Arteta na kuongeza kuwa kocha huyo ana sifa zote zinazomfaa kocha wa kuwa kwenye Ligi Kuu England.
“Kama anafanya kazi kwenye Ligi ya Mabingwa, michuano ambayo ni mikubwa zaidi Ulaya, maana yake ni kwamba anaweza kufanya kazi popote,” alisema Arteta ambaye timu yake leo Jumanne, Oktoba 21, inaumana na Atletico
