Na mwandishi wetu
Simba imeuwasha moto ugenini kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuichapa Nsingizini Hotspur ya Eswatini katika mechi iliyochezwa Jumapili hii Oktoba 19, 2025 kwenye dimba la Somhololo.
Wenyeji Nsingizini licha ya kuonesha dalili za umakini katika kukabiliana na kasi ya hawakuweza kumaliza kipindi cha kwanza salama baada ya kupachikwa bao dakika ya 45 lililofungwa na beki Wilson Nangu kwa shuti lililomshinda mlinda mlango wa Nsingizini.
Kipindi cha pili timu zote zilionesha uhai Simba ikisaka bao la nyongeza wakati wenyeji Nsingizi wakitafuta la kusawazisha lakini walikuwa ni Simba waliofanikisha azma yao katika dakika 10 za mwisho za mcheza huo.
Simba waliandika bao la pili dakika ya 84 mfungaji akiwa ni Kibu Dennis, bao ambalo lilionekana dhahiri kuwaumiza Nsingizini ambao walijikuta wakichapwa bao la tatu dakika sita baadaye na kwa mara nyingine bao hilo lilifungwa na Kibu.
Matokeo hayo yanakuwa kete nzuri kwa Simba kusonga mbele hatua ya makundi baada ya mechi ya marudiano baina ya timu hizo inayotarajia kupigwa juma lijalo jijini Dar es Salaam ambapo Nsingizini watahitaji ushindi wa zaidi ya mabao matatu ili kusonga mbele.
Kimataifa Simba shujaa ugenini
Simba shujaa ugenini
Read also
