Madrid, Hispania
Mshambuliaji wa Real Madrid, Kylian Mbappé amesema Cristiano Ronaldo bado ni namba moja katika klabu hiyo akimtaja nyota huyo mwenye rekodi ya wakati wote ya mabao kuwa ni mfano wa kuigwa na amekuwa akipata ushauri kutoka kwake.
Ronaldo, mmoja wa mastaa waliomvutia Mbappe tangu akiwa mdogo ana rekodi ya kufunga mabao 450 katika misimu tisa aliyoichezea Real Madrid kati ya mwaka 2009 hadi 2018 akiwa pia ameshinda mataji 16 yakiwamo manne ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Mbappe kwa sasa ana matumaini ya kufuata nyayo za Ronaldo akiwa tayari amefunga mabao 44 katika msimu wake wa kwanza na Real Madrid wa 2024-25 na katika msimu huu wa 2025-26 ambao ni wa pili kwa mchezaji huyo, hadi sasa ameifungia timu hiyo mabao 14.
“Cristiano kwangu kwa wakati wote amekuwa mfano wa kuigwa,, nina bahati ya kipekee kuweza kuwasiliana naye, ananisaidia na ananipa ushauri nafikiri kwa Madrid yeye bado ni namba moja,” alisema Mbappe.
Mbappe pia alisema kwamba Ronaldo pia ni mtu wa kufanyia marejeo kwa wachezaji wanapokuwa na jambo lao wakati mashabiki bado wanamuota na yeye (Mbappe) akisisitiza kwamba anataka kufuata nyayo za mchezaji huyo.
Kwa upande mwingine Mbappe pia aliizungumzia timu yake ya taifa ya Ufaransa ambayo inatajwa kuwa moja ya timu zinazoweza kubeba Kombe la Dunia 2026 ingawa mchezaji huyo pia anaamini Hispania ni moja ya timu shindani zilizo vizuri.
Mbappe ambaye akiwa na Ufaransa alibeba Kombe la Dunia mwaka 2018, alisema anaamini HIspania ni timu bora Ulaya kwa wakati huu ingawa alitahadharisha kuwa Kombe la Dunia ni michuano tofauti.
Kimataifa Mbappe: Ronaldo hana mpinzani
Mbappe: Ronaldo hana mpinzani
Read also
