Manchester, England
Klabu ya Manchester United inadaiwa kuwa katika mkakati wa kumrudisha England, mshambuliaji wa zamani wa Tottenham Hotspur, Harry Kane ambaye kwa sasa anaichezea Bayern Munich ya Ujerumani.
Kane, 32 ambaye pia ni mshambuliaji nyota na nahodha wa timu ya taifa ya England alijipatia mafanikio kwa kuweka rekodi za kutisha za mabao akiwa na Tottenham kabla ya kuihama timu hiyo na kujiunga na Bayern misimu miwili iliyopita.
Habari za Man United kumtaka mshambuliaji huyo zimechangiwa kwa kiasi kikubwa na kinachodaiwa kwamba huenda Kane akaachana na Bayern majira yajayo ya kiangazi na hiyo kuwa fursa nzuri kwa mchezaji huyo kurudi England.
Wakati Man United ikionesha shauku hiyo, kocha wa Tottenham Thomas Frank anatambua kila kinachoendelea na anamkaribisha mshambuliaji huyo kurudi kwa mara nyingine katika klabu hiyo ya London ingawa anatambua kuwa uwezekano wa Kane kuachana na Bayern ni mdogo.
Kane baada ya kuweka rekodi mbalimbali za mabao akiwa na Spurs alikuwa pia akiwindwa na klabu kadhaa barani Ulaya ikiwamo PSG ya Ufaransa lakini mwenyewe akaichagua Bayern ambapo ameendelea kuonesha uwezo wake wa kuzifumania nyavu.
Kimataifa Man Utd yamtolea macho Kane
Man Utd yamtolea macho Kane
Read also
