Na mwandishi wetu
Baada ya kuwapo kuhusu katibu mkuu wa Shirkisho la Soka Tanzania (TFF), Wilfred Kidau kuachia ngazi, hatimaye kila kitu kimewekwa wazi baada ya shirikisho hilo kumteua Oscar Mirambo (pichani) kushika nafasi ya Kidau.
Taarifa ya TFF iliyopatikana leo Jumatano, Septemba 24, 2025 hata hivyo ilieleza kuwa Kidau ameondoka katika nafasi hiyo baada ya mkataba wake kufikia ukomo na si vinginevyo.
Katika taarifa hiyo, TFF hata hivyo hawakuweka wazi iwapo Kidau alikataa kuongeza mkataba au TFF haikuwa tayari kumuongezea mkataba badala yake kilichoelezwa ni kuwa kamati ya utendaji ya TFF ndiyo iliyofikia uamuzi huo.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Mirambo ataanza rasmi kazi hiyo, Oktoba Mosi wakati mkataba wa Kidau na TFF unafikia ukomo Septemba 30.
Kidau ambaye ni muajiriwa wa TFF na mchezaji wa zamani wa soka, aliingia madarakani mwaka 2014 mara baada ya Wallace Karia kuchaguliwa mara ya kwanza kuwa rais wa TFF ingawa haikuwahi kuwekwa wazi kuhusu mkataba wa Kidau na TFF.
Soka Mirambo amrithi Kidau TFF
Mirambo amrithi Kidau TFF
Related posts
Read also
