Na mwandishi wetu
Timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ imetoka sare ya bila kufungana na Jamhuri ya Afrika ya Kati katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ligi za ndani (CHAN).
Matokeo ya mechi hiyo ya mwisho ya hatua ya makundi iliyochezwa Jumamosi Agosti 16, 2025 kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam yanaifanya Stars kumaliza hatua hiyo ikiwa kinara wa Kundi B.
Stars kabla ya mechi hiyo ilikuwa tayari imefuzu hatua ya robo fainali, katika kundi hilo lenye timu tano imeshinda mechi tatu na kutoka sare moja na hivyo kufikisha pointi 10.
Timu ya Madagascar ambayo imeifunga Burkina Faso mabao 2-1, imeshika nafasi ya pili ikiwa na pointi saba na hivyo kuungana na Stars katika hatua ya robo fainali.
Nafasi ya tatu katika kundi hilo inashikiliwa na Mauritania ambayo pia ina pointi saba sawa na Madagascar lakini Madagascar ina faida ya uwiano mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa.
Kimataifa Stars, Afrika ya Kati hakuna mbabe
Stars, Afrika ya Kati hakuna mbabe
Read also
