Na mwandishi wetu
Kampuni ya michezo ya kubahatisha ya SportPesa ya Tanzania imesaini mkataba mpya wa udhamini wa miaka mitatu na klabu ya Yanga, mkataba wenye thamani ya Sh bilioni 21.7.
Mkataba huo mpya unakuwa ni mwendelezo wa mahusiano mazuri kati ya Yanga na SportPesa ambao mwaka 2022 walisani mkataba wa miaka mitatu uliokuwa na thamani ya Sh bilioni 12.3 ambao umefikia tamati mwaka huu.
Katika mkataba mpya uliotangazwa rasmi Jumatatu hii Agosti 11, 2025, Yanga watakuwa wakipokea kiasi cha Sh bilioni 7.2 kwa kila mwaka.
Akizungumza wakati wa hafla ya kusaini mkataba huo, Mkurugenzi wa SportPesa, Tarimba Abbas alisema iwapo Yanga itatwaa ubingwa wa Afrika, kampuni yao itatoa zawadi ya kipekee ambayo haijawahi kutolewa kwa klabu yoyote Afrika.
Naye, meneja habari na mawasiliano Yanga, Ally Kamwe akizungumza wakati wa hafla hiyo alisema kwamba makubaliano yao na SportPesa yamekuwa gumzo kubwa kwa siku ya jana.
“Tumeliteka taifa, tulitangaza kuwa tumepokea ofa tukaikataa, lakini baadaye tukapokea ofa nyingine kubwa tukaikubali, ofa hiyo ni udhamini mkubwa na wa kihistoria kutoka kwa SportPesa,” alisema Kamwe.
Soka SportPesa yaongeza pesa Yanga
SportPesa yaongeza pesa Yanga
Read also
