Na mwandishi wetu
Katika kujiimarisha kwa ajili ya msimu mpya wa Ligi Kuu NBC wa 2025-26 na michuano ya kimataifa, Azam FC imemsajili kiungo wa zamani wa Simba, Sadio Kanoute.
Kanoute ambaye aliichezea Simba kabla ya kuachana nayo mara tu baada ya kumalizika kwa msimu wa 2023-24, alisifika kwa upambanaji wake lakini ghafla Simba waliachana naye.
Baada ya kuachana na Simba, Kanoute alijiunga na JS Kablie ya Algeria ambayo hata hivyo aliichezea kwa msimu mmoja kabla ya kurudi tena Tanzania na kujiunga na Azam.
Akizungumzia kujiunga kwake na Azam, Kanoute ambaye ametangazwa rasmi na timu hiyo Jumatatu hii Agosti 11, 2025 alisema, “Nimefurahi kujiunga na Azam, niko tayari kujitoa kwa kila kitu kwa ajili ya klabu hii na mashabiki wake.”
Mbali na Simba na Kablie, Kanoute si jina geni katika soka la Afrika kwani mbali na kwao Mali alikochezea timu kadhaa, pia amewahi kukipiga nchini Libya na klabu ya Al Ahly Benghazi.
Alisajiliwa na Simba mwaka 2021 na kuwa mmoja wa wachezaji tegemeo katika michuano ya kimataifa pamoja na Ligi Kuu NBC akiwa mwenye uhakika wa namba mara kwa mara kwenye kikosi cha kwanza.
Soka Sadio Kanoute aibukia Azam
Sadio Kanoute aibukia Azam
Related posts
Read also
