Na mwandishi wetu
Timu za Yanga na Simba zimewajua wapinzani wao kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika msimu wa 2025-26, Yanga wataanza na Benguela FC ya Angola na Simba dhidi ya Gaborone Utd ya Botswana.
Kwa mujibu wa droo iliyofanyika jijini Dar es Salaam, leo Jumamosi Agosti 9, 2025, timu nyingine ya Tanzania Mlandege kutoka visiwani Zanzibar itaumana na Ethiopia Insuarance ya nchini Ethiopia.
Timu zote za Tanzania kwenye michuano hiyo inayoandaliwa na kusimamiwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) zitaanzia katika hatua za awali na mechi zote za kwanza zitachezwa kati ya Septemba 19 hadi 21.
Kwa upande wa Yanga baada ya mechi hiyo iwapo itashinda mtihani huo wa kwanza, itaumana na mshindi wa mechi kati ya Elgeco ya Madagascar na Silver Strikers ya Malawi.
Kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, Azam FC itaanza kwa kuikabili Al Meriekh Bentui ya Sudan Kusini wakati Singida BS itaumana na Rayon Sport ya Rwanda huku KMKM ya Zanzibar ikivaana na AS Sport ya Djibout.
Katika hatua inayofuata ya Kombe la Shirikisho, mshindi wa mechi ya Azam na Meriekh ataumana na mshindi kati ya KMKM na AS Sport.
Mshindi kati ya Rayon na Singida atakabiliana na mshindi wa mechi kati ya Flambeau ya Burundi na timu kutoka Libya itakayojulikana hapo baadaye.
Kimataifa Yanga, Simba zawajua wapinzani CAF
Yanga, Simba zawajua wapinzani CAF
Read also
