London, England
Kiungo wa zamani wa Arsenal, Thomas Partey amepewa dhamana yenye masharti baada ya kukata rufaa katika kesi ya kubaka na kudhalilisha kijinsia inayomkabili.
Partey, 32, anadaiwa kufanya makosa hayo kati ya mwaka 2021 na 2022 wakati huo akiwa mchezaji wa Arsenal.
Mchezaji huyo ambaye pia anaichezea timu ya taifa ya Ghana, ameshitakiwa kwa makosa matano ya kubaka wanawake wawili na makosa mengine ya udhalilishaji kijinsia dhidi ya mwanamke mmoja.
Partey aliingia Mahakama ya Westminster jana Jumanne akiwa amevaa nguo yenye rangi nyeusi, katika masharti ya dhamana ametakiwa kutowasogelea karibu wanawake anaodaiwa kuwafanyia udhalilishaji huo.
Mahakama hiyo pia imemtaka mchezaji huyo kuiarifu polisi wakati wowote atakapotaka kusafiri safari za kimataifa na pia atatakiwa kutoa taarifa pale atakapoamua kubadili makazi.
Awali polisi walidai kupewa taarifa za tuhuma za kubaka na udhalilishai, Februari 2022, lakini mwanasheria wa mchezaji huyo alikana makosa yote na kudai kwamba anaisubiri siku ya kusafisha jina la mtuhumiwa.
Kadhia inayomkabili mchezaji huyo imekuja wakati kukiwa na habari kwamba yupo mbioni kujiunga na klabu ya Villarreal ya Hispania.
Kimataifa Kiungo Arsenal apewa dhamana kesi ya kubaka
Kiungo Arsenal apewa dhamana kesi ya kubaka
Read also
