Barcelona, Hispania
Mshambuliaji wa Man United, Marcus Rashford yuko nchini Hispania kwa ajili ya kukamilisha mipango ya kujiunga kwa mkopo na timu ya Barcelona.
Rashford, 27, aliwasili katika Barcelona, jana Jumapili usiku baada ya kupewa ruhusa na Man United kwa ajili ya kukamilisha mipango ya kujiunga na klabu hiyo.
Picha za mchezaji huyo akiwasili katika jiji la Barcelona na ndege binafsi zilizagaa kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii na vyanzo mbalimbali vya habari.
Mazungumzo kati ya Man United na Barcelona au Barca yanadaiwa kwenda vizuri wiki iliyopita huku makubaliano ya mambo ya msingi yakifikiwa na pande hizo mbili na habari zaidi zikidai kuwa mchezaji huyo atasajiliwa kwa mkopo wa miezi 12.
Rashford ambaye pia ni mchezaji wa timu ya taifa ya England, mekuwa akitamani changamoto mpya na amewahi kunukuliwa hivi karibuni akisema kwamba angependa kucheza timu moja na staa wa Barca, Lamine Yamal.
Hii itakuwa mara ya pili kwa Rashford kuondoka Man United na kujiunga na timu nyingine kwa mkopo, msimu uliopita alicheza kwa mkopo wa miezi sita akiwa na klabu ya Aston Villa.
Rashford anatarajia kufanyiwa vipimo vya afya wakati wowote wiki hii ili aweze kujiunga na kikosi cha Barca kwa ajili ya ziara ya maandalizi ya msimu mpya wa 2025-26 katika nchi za Japan na Korea Kusini.
Mipango ya Rashford kujiunga na Barca ikikamilika, mchezaji huyo atakutana na nyota mwenzake wa zamani wa Man United, Jesse Lingard ambaye kwa sasa anaichezea timu ya FC Seoul ya Korea Kusini, timu ambayo Julai 31 itacheza na Barca.
Kimataifa Rashford atua Barcelona
Rashford atua Barcelona
Read also
