Riyadh, Saudi Arabia
Klabu ya Al Ahli ya Saudi Arabia inatajwa kuwa na mkakati mzito wa kumsajili nyota wa Inter Miami ya Marekani Leonel Messi ambaye mkataba wake na klabu hiyo unafikia ukomo baadaye mwaka huu.
Kwa mujibu wa chanzo kimoja cha habari, Ahli wanataka kufanya kile liwezekanalo ili kuhakikisha wanamshawishi nyota huyo wa zamani wa Barcelona na PSG akubali kusaini timu hiyo.
Kwa kutambua kwamba mkataba wa Messi na klabu hiyo ya Marekani imebakisha miezi isiyozidi mitano, Ahli wameamua kuanza mapema mazungumzo na wawakilishi wa Messi.
Messi ambaye pia ni nahodha wa timu ya taifa ya Argentina, jina lake si geni nchini Saudi Arabia kwani ni balozi wa Bodi ya Utalii Saudi Arabia hivyo itakuwa vizuri kwa Ahli kumsajili nyota huyo.
Inter Miami nao pengine kwa kutambua ushawishi ambao mchezaji huyo anaupata kutoka Saudi Arabia inadaiwa nao wameshaanza taratibu za kumuongezea mkataba mchezaji huyo.
Barcelona, timu ambayo Messi ameichezea kwa mafanikio zaidi iliwahi kutajwa kumtaka mchezaji huyo wakati anaondoka PSG lakini Messi hakuwa tayari kurudi katika klabu hiyo aliyoanza kuichezea kwenye akademi yao.
Kimataifa Ahli yapania kumsajili Messi
Ahli yapania kumsajili Messi
Read also
