London, England
Kocha wa England, Thomas Tuchel amewataka wachezaji kucheza kama wanapokuwa mazoezini kwa kucheza wakiwa na nyuso za furaha wakati wakijiandaa kuivaa Senegal, leo Jumanne, Juni 10, 2025.
Tuchel, alionekana kutofurahia uchezaji wa timu yake licha ya ushindi wa bao 1-0 ambao timu hiyo iliupata dhidi ya Andorra katika mechi ya kufuzu fainali za Kombe la Dunia, Jumamosi iliyopita.
Kocha huyo wa zamani wa Chelsea alisema kwamba wachezaji wake walifanya mazoezi tofauti na sasa amewataka kucheza wakiwa huru na kufuata maelekezo.
Tuchel ambaye ni Mjerumani, alianza kazi ya kuinoa England Januari mwaka huu na mechi ya leo ya kirafiki dhidi ya Senegal ni mechi yake ya nne akiwa na timu hiyo.
“Naona tunafanya mazoezi tukiwa na tabasamu lakini hatuchezi mechi tukiwa na tabasamu, kwa hakika tunahitaji kuwa bora zaidi, tunatakiwa kuchangamka katika kundi letu, naona kama tunajitenga uwanjani,” alisema Tuchel.
Tuchel aliongeza kwa kusema kwamba timu hiyo ina mambo mengi mazuri ya kuyafanya nje ya uwanja wa mazoezi ambayo amekuwa akiyaona na kinachotakiwa ni kuhakikisha yote yanahamia uwanjani wakiwa kwenye mechi.
“Jambo la muhimu ni kuweka umakini katika kanuni za mchezo, kupeana maelekezo sahihi miongoni mwa wachezaji na kile tunachokitarajia katika majukumu yao,” alisema Tuchel.
Kimataifa Tuchel ataka England wacheze kwa raha zao
Tuchel ataka England wacheze kwa raha zao
Read also
