na mwandishi
Simba imetolewa katika Kombe la Shirikisho CRDB baada ya kulala kwa mabao 2-1 mbele ya Singida Black Stars katika mechi ya nusu fainali iliyopigwa Jumamosi hii Mei 31, 2025 kwenye Uwanja wa Tanzanite Kwaraa mjini Manyara.
Kipigo hicho kinaifanya Simba kutolewa katika mbio za kulisaka taji hilo na sasa imebakiwa na taji moja tu la Ligi Kuu NBC baada ya kushindwa kutamba mbele ya RS Berkane kwenye Kombe la Shirikisho Afrika.
Singida BS walianza mapema kulichachafya lango la Simba na kuandika bao la kwanza katika dakika ya 17 mfungaji akiwa Jonathan Sowah ambaye alifunga bao hilo kupitia pasi ya Arthur Bada.
Dakika 10 baada ya bao hilo, Simba walipata pigo kwa kipa wao namba moja, Musa Camara kuumia alipogongana na Sowah na hivyo kutolewa nje na nafasi yake kuingia Ally Salim.
Mambo yalizidi kuwa mabaya kwa Simba kwani dakika saba baada ya kuingia kwa kipa huyo, Singida waliandika bao la pili lililofungwa na Emmanuel Keyekeh.
Keyekeh alifunga bao hilo akiyatumia makosa ya kipa Salim ambaye alirudisha mpira vibaya na kumkuta mfungaji ambaye hakufanya ajizi kufumua shuti lililojaa wavuni.
Keyekeh alikamilisha karamu ya mabao ya Singida dakika ya tatu baada ya kuanza kipindi cha pili kwa kufunga bao lililotokana na mpira wa adhabu.
Adhabu hiyo ilitolewa na mwamuzi Ahmed Arajiga baada ya Edmund John kuchezewa rafu akiwa nje kidogo ya eneo la 18 na ndipo Keyekeh alipopiga mpira uliokwenda moja kwa moja hadi wavuni
Baada ya mabao hayo, Singida waliimarisha ulinzi lakini Simba walipambana na kupata bao pekee la kufutia machozi dakika ya 68 lililofungwa na Jean Ahoua kwa mpira wa adhabu uliotokana na rafu aliyochezewa Elly Mpanzu.
Mechi ya fainali ya michuano hiyo kati ya Singida na Yanga inatarajiwa kupigwa kati ya Juni 26 na 28 mwaka huu.
Soka Singida BS yaitoa Simba Shirikisho CRDB
Singida BS yaitoa Simba Shirikisho CRDB
Read also
