Liverpool, England
Mshambuliaji wa Liverpool, Mohamed Salah ametangazwa kuwa nyota wa msimu wa 2024-25 wa Ligi Kuu England (EPL).
Mara ya kwanza Salah kubeba tuzo hiyo ambayo mshindi wake hupatikana kupitia kura zinazopigwa zikihusisha mashabiki na wataalam wa soka, ilikuwa msimu wa 2017-18.
Salah, 32 ambaye ameiongoza Liverpool kubeba taji la EPL msimu huu aliwashinda wachezaji wenzake wa Liverpool Virgil van Dijk na Ryan Gravenberch ambaye ametwaa tuzo ya mchezaji bora kijana wa msimu.
Wengine waliokuwa wakiwania tuzo hiyo na Salah ni Declan Rice wa Arsenal, Alexander Isak wa Newcastle, Bryan Mbeumo wa Brentford pamoja na Morgan Gibbs-White na Chris Wood wa Nottingham Forest..
Hii pia inakuwa mara ya kwanza tangu msimu wa 2018-19 kwa mchezaji wa Man City kutobea tuzo ya msimu husika.
Kesho Jumapili. Salah ataingia uwanjani kucheza mechi ya mwisho ya msimu dhidi ya Crsytal Palace huku tayari akiwa amezifumania nyavu mara 28 ambayo ni mabao matano kumzidi Alexander Isak wa Newcastle.
Msimu huu pia Salah ameumaliza kwa kuweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kigeni mwenye mabao mengi zaidi katika historia ya EPL akiwa amemzidi Sergio Aguero aliyekuwa akishikilia rekodi hiyo.
Salah ambaye mwezi huu pia alitangazwa kuwa mchezaji bora na Chama cha Waandishi wa Habari za Soka pia ameongeza miaka miwili katika mkataba wake ambao sasa utamfanya aendelee kuwa na Liverpool hadi mwaka 2027.
Kimataifa Salah nyota wa msimu EPL
Salah nyota wa msimu EPL
Read also
