London, England
Arsenal wamefurahia kurejea dimbani kwa mshambuliaji wao Bukayo Saka aliyekuwa majeruhi kwa takriban miezi mitatu lakini hapo hapo wamepata pigo jingine baada ya kuumia kwa beki wao wa kati Gabriel.
Saka amerejea na kufunga bao jana Jumanne katika mechi dhidi ya Fulham, mechi ambayo Arsenal ilitoka na ushindi wa mabao 2-1 na kujinyakulia pointi tatu muhimu.
Haikushangaza kwa mashabiki wa Arsenal kumpa heshima Saka kwa kumshangilia kwa kusimama mara baada ya jina lake kutajwa uwanjani japo hali ni tofauti kwa kocha Mikel Arteta.
Kwa Arteta ushindi huo na kurejea kwa Saka ilikuwa furaha ya muda tu, hali bado tete, wachezaji majeruhi wanaendelea kumpa mtihani wa kupanga kikosi chake.
Kuhusu Gabriel, beki wa kati Mbrazil alipata matatizo ya misuli kipindi cha kwanza katika mechi ya jana na hivyo ni wazi ataikosa mechi ya pili ya robo fainali Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Real Madrid Jumanne ijayo.
Hali ni hiyo hiyo kwa mshambuliaji Kai Havert ambaye msimu huu umekuwa wa hovyo kwake baada ya kupatwa na matatizo ya misuli.
Kama hiyo haitoshi, beki Jurrien Timber naye alilazimika kukaa pembeni katika mechi ya jana dhidi ya Fulham akikabiliwa na tatizo la goti kama ilivyo kwa Ricardo Calafiori na Ben White ambao kila mmoja ana tatizo la goti.
Arteta ana kazi kubwa ya kufanya licha ya kuwa na wachezaji wake muhimu ni majeruhi, kazi mbili zilizo mbele yake zote ni ngumu.
Kwanza katika Ligi Kuu England (EPL) timu yake inashika nafasi ya pili, anatakiwa kuishusha kileleni Liverpool inayoshika usukani wakati kwenye Ligi ya Mabingwa mtihani wa robo fainali dhidi ya Real Madrid si mdogo.
Kimataifa Majeruhi Arsenal wamtesa Arteta
Majeruhi Arsenal wamtesa Arteta
Read also
