London, Englaned
Kocha wa zamani wa Chelsea na Bayern Munich, Thomas Tuchel, leo Januari Mosi, 2025 ameanza rasmi kazi yake mpya ya kuinoa timu ya taifa ya England akiwa na mkataba wa miezi 18.
Tuchel ambaye Oktoba mwaka jana, alitangazwa rasmi kuchukua nafasi hiyo iliyokuwa ikishikliwa na Gareth Southgate ataiongoza timu hiyo hadi baada ya fanali za Kombe la Dunia 2026.
Ikiwa na Southgate, England ilifikia hatua ya fainali ya Kombe la Ulaya 2024 au Euro 2024 nchini Ujerumani lakini licha ya matarajio makubwa timu hiyo ilishindwa kutamba mbele ya Hispania waliobeba taji hilo.
Katika kibarua hicho kipya, Tuchel atakuwa akisaidiwa na Anthony Barry ambaye pia amefanya naye kazi tangu akiwa Chelsea na baadaye Bayern Munich.
England kwenye kusaka tiketi ya kushiriki fainali za Kombe la Dunia 2026 imepangwa kundi moja na timu za Serbia, Latvia, Albania na Andora.
Kati ya timu hizo, Tuchel ambaye pia amewahi kuzinoa timu za Borussia Dortmund ya Ujeruani na PSG ya Ufaransa alisema anaziheshimu Serbia na Albania ambazo alisema zina uwezo wa kuibua mshangao.
Kibarua cha kwanza kwa Tuchel na timu ya England kwenye kufuzu Kombe la Dunia 2026 kitakuwa Machi 21 mwaka huu dhidi ya Albania na siku tatu baadaye dhidi ya Latvia mechi ambazo zitapigwa kwenye dimba la Wembley.
Mara baada ya kuondoka kwa Southgate, England imekuwa chini ya kocha wa muda, Lee Carsey ambaye ana rekodi ya kushinda mechi tano kati ya sita.
Kimataifa Tuchel aanza kibarua England
Tuchel aanza kibarua England
Read also
