Stockholm, Sweden
Waendesha mashitaka wa Sweden leo Alhamisi wametangaza kufuta uchunguzi ulioanzishwa wa tuhuma za kubaka alizokuwa akihusishwa nazo mshambuliaji wa Real Madrid, Kylian Mbappe.
Kwa mujibu ya taarifa ya waendesha mashitaka hao, uamuzi wa kufuta uchunguzi huo umekuja baada ya kubaini kuwa hakuna ushahidi wa kutosha kuendelea na uchunguzi.
Tuhuma hizo zilimhusisha Mbappe ambaye alidaiwa kufanya tukio hilo katika hoteli moja ya jijini Stockholm.
Katika tukio hilo ilielezwa kuwa kulikuwa na mtu alihusishwa na tukio la kubaka na wawili waliohusishwa na tukio la udhalilishwaji kijinsia lakini hakujawa na ushahidi wa kutosha kuendelea na uchunguzi wa tukio hilo na hivyo uchunguzi huo umefutwa.
Taarifa ya waendesha mashitaka hao haikumtaja mtuhumiwa wa kadhia hiyo lakini vyanzo kadhaa vya habari nchini Sweden vilimtaja mshambuliaji huyo wa Real Madrid ambaye alitembelea jiji la Stockholm wakati wa mapumziko mwezi Oktoba.
Chanzo kimoja cha habari kimeeleza kuwa awali wakili wa Mbappe alizipuuza tuhuma hizo akidai kuwa ni za uwongo ingawa baada ya uamuzi wa kufuta uchunguzi, wakili huyo hakutoa taarifa yoyote.
Mbappe ambaye pia ni nahodha wa timu ya taifa ya Ufaransa, alijiunga na Real Madrid mwanzoni mwa msimu huu akitokea PSG ya Ufaransa.
Kimataifa Mbappe asafishwa kesi ya kubaka
Mbappe asafishwa kesi ya kubaka
Read also
