Barcelona, Hispania
Shubiri inafahamika kwa uchungu na ndicho kilichomkuta mshambuliaji wa Real Madrid, Kylian Mbappe, Jumamosi hii alipocheza mechi yake ya kwanza dhidi ya Barcelona maarufu El Clasico na kujikuta pagumu baada ya timu yake kubugizwa mabao 4-0.
Mbappe ambaye huu ni msimu wake wa kwanza Real Madrid tangu ajiunge na timu hiyo akitokea PSG, kwa mara ya kwanza alicheza mechi hiyo kubwa ya El Clasico lakini ukawa mwanzo mbaya.
Kwa Mbappe bila shaka aliingia katika mechi hiyo akikumbuka mabao matatu (hat trick) ambayo aliwafunga Barca, Februari 2021 na kuiwezesha PSG kutoka na ushindi wa 4-1 katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Mbappe hata hivyo alishindwa kufanya jambo linalofanana na hilo baada ya kuwa na wakati mgumu Jumamosi katika uwanja huo huo wa Nou Camp ambao mwaka 2021 alitoka kifua mbele na mabao matatu.
Kushindwa kwa Mbappe kutamba katika El Clasico kunatajwa kuwa ni mwendelezo wa mwanzo usio wa kuvutia kwa mshambuliaji huyo tishio duniani ambaye katika mechi zake tatu za awali za La Liga alitoka uwanjani bila bao.
Mbappe pia tangu aanze kuivaa jezi ya Real Madrid hadi sasa ana mabao sita tu katika La Liga jambo ambalo halikutarajiwa hasa kutokana na matarajio makubwa yaliyokuwapo kabla ya usajili wake haujakamilika.
Mchezaji mwingine wa Real Madrid anayepitia wakati mgumu ni Jude Bellingham ambaye msimu uliopita ambao pia ulikuwa wa kwanza kwake, alikuwa moto akitupia wavuni mabao 19 lakini kwa msimu huu hadi sasa hana bao hata moja.
Kimataifa Mbappe aonja shubiri El-Clasico
Mbappe aonja shubiri El-Clasico
Read also
