Beijing, China
Wanasoka 38 na maofisa watano wa klabu za soka nchini China wamefungiwa kujihusisha na soka kwa maisha yao yote baada ya kukutwa na hatia ya upangaji matokeo, rushwa na uchezaji kamari.
Ofisa Mwandamizi Wizara ya Usalama wa Ndani nchini China, Zhang Xiaopeng alisema uchunguzi walioufanya kwa miaka miwili ulibaini matukio 128 ya upangaji matokeo ukihusisha watuhumiwa 128 na maofisa 41 na klabu za soka.
Miongoni mwa waliokumbana na adhabu hiyo wamo wanasoka wa zamani wa kimataifa wa China, Guo Tianyu, Gu Chao na Jin Jingdao na mchezaji wa Korea Kusini, Son Jun-ho ambao sasa hawana ruhusa ya kujihusisha na masuala yoyote ya soka kwa maisha yao yote.
Son alikamatwa akiwa China na kutiwa ndani kwa miezi 10 kabla ya kuachiwa Machi mwaka huu na kurejea kwao Korea Kusini na kwa sasa anaichezea klabu ya Suwon kwa kile ambacho uongozi wa klabu hiyo unadai kwamba adhabu ya mchezaji huyo inafanya kazi China pekee.
Rais wa Chama cha Soka China (CFA), Song Kai (pchani) alisema kuwa watu hao wanakabiliwa na adhabu zinazotokana na makosa ya jinai na wamefungiwa maisha kujihusisha na masuala ya soka.
Kwa mujibu wa Kai miongoni mwa waliokumbwa na adhabu hiyo wapo wachezaji 17 na maofisa wawili wa klabu waliofungiwa kwa miaka mitano akiwamo mchezaji wa kimataifa wa Cameroon, Ewolo Donovan ambaye anaichezea klabu ya Heilongjiang Ice City.
Kai pia alimtaja mchezaji wa zamani wa timu ya Hangzhou Greentown, Shen Liuxi ambaye licha ya kuwa ni mtuhumiwa lakini hayumo kwenye adhabu ya kifungo cha maisha kwa sababu tayari anatumikia adhabu hiyo tangu mwaka 2013.
Katika uchunguzi mpya, Kai alisema kwamba mchezaji huyo alikutwa na hatia ya matukio ya upangaji matokeo na kufungua casino kinyume na utaratibu
China imekuwa katika mkakati mzito wa kukabiliana na matukio ya rushwa na upangaji matokeo ambapo Machi mwaka huu rais wa zamani wa CFA alipewa adhabu ya kifungo cha jela maisha kwa kosa la kupokea rushwa na kujihusisha na upangaji wa matokeo.
Takriban miezi mitano baada ya adhabu hiyo makamu rais wa zamani wa CFA alipewa adhabu ya kifo ch jela miaka 11 kwa kosa la kupokea rushwa pamoja na mkurugenzi wa zamani wa mashindano wa CFA naye alifungwa jela miaka saba kwa kosa hilo hilo.
Kimataifa 43 wafungiwa maisha China kwa kupanga matokeo
43 wafungiwa maisha China kwa kupanga matokeo
Read also
