Monaco, Ufaransa
Real Madrid itazianza kampeni za kulitetea taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya ugenini dhidi ya Liverpool katika mfumo mpya wa michuano hiyo ambao umefuta utaratibu wa timu kuanzia hatua ya makundi.
Kwa mujibu wa droo iliyofanywa leo Alhamisi na Uefa, timu nyingine za England za Man City na Arsenal zote zitacheza na PSG wakati Aston Villa itakuwa na Celtic ambao ni mabingwa wa Scotland.
Katika mfumo huo mpya utakaoanza msimu huu wa 2024-25 kwa wanaume ukiwa na timu 36, kila timu itacheza mechi nane za awali, nne nyumbani na nne ugenini na mechi za kwanza zitachezwa kati ya Septemba 17 na 19 mwaka huu.
Kwa mujibu wa mfumo huo mpya, idadi ya mechi sasa zitaongezeka kutoka 125 za awali hadi 189 wakati timu 16 za juu zitacheza hatua ya 16 bora.
Namna ratiba ya kila mechi itakavyokuwa itajulikana keshokutwa Jumamosi baada ya droo za michuano mingine ya klabu barani Ulaya ya Europa Ligi na Conference Ligi kufanyika lakini hadi sasa kila timu inawajua wapinzani wake kama ifuatavyo…
Aston Villa
Bayern Munich (H)
Leipzig (A)
Juventus (H)
Club Bruges (A)
Celtic (H)
Young Boys (A)
Bologna (H)
Monaco (A)
Arsenal
Paris St-Germain (H)
Inter Milan (A)
Shakhtar Donetsk (H)
Atalanta (A)
Dinamo Zagreb (H)
Sporting Lisbon (A)
Monaco (H)
Girona (A)
Celtic
Aston Villa (A)
Leipzig (H)
Borussia Dortmund (A)
Club Bruges (H)
Atalanta (A)
Young Boys (H)
Dinamo Zagreb (A)
Slovan Bratislava (H)
Liverpool
Real Madrid (H)
Leipzig (A)
Leverkusen (H)
AC Milan (A)
Lille (H)
PSV Eindhoven (A)
Bologna (H)
Girona (A)
Manchester City
Inter Milan (H)
Paris St-Germain (A)
Club Brugge (H)
Juventus (A)
Feyenoord (H)
Sporting Lisbon (A)
Sparta Prague (H)
Slovan Bratislava (A)
Kimataifa Real Madrid kuikabili Liverpool Ligi ya Mabingwa
Real Madrid kuikabili Liverpool Ligi ya Mabingwa
Read also
