Na mwandishi wetu
Simba leo Jumapili imeibugiza Fountain Gate mabao 4-0 katika mechi ya Ligi Kuu NBC iliyopigwa kwenye dimba la KMC Complex jijini Dar es Salaam.
Bao la kwanza la Simba lilipatikana dakika ya 13 ya mchezo huo mfungaji akiwa ni Edwin Balua ambaye aliitumia pasi ya nyota mpya wa timu hiyo, Jean Ahoua kuipatia Simba bao la awali.
Kuingia kwa bao hilo kulichochea kasi ya mashambulizi kwa Simba ambao dakika moja kabla ya timu kwenda mapumziko waliandika bao la pili mfungaji akiwa ni Steven Mukwala aliyeitumia pasi ya Shomary Kapombe.
Dakika 15 baada ya kuanza kipindi cha pili, Ahoua aliifungia Simba bao la tatu akiitumia pasi ya Mohammed Hussein ‘Zimbwe Junior’ kuandika bao hilo ambalo pia ni bao lake la kwanza tangu ajiunge na Simba.
Karamu ya mabao ya Simba ilikamilishwa na Valentino Mashaka ambaye alifunga bao la nne akiitumia pasi ya Ahoua.
Katika mechi nyingine ya ligi hiyo iliyopigwa leo, Namungo ikiwa nyumbani ilishindwa kutamba mbele ya Tabora United baada ya kulala kwa mabao 2-1.
Soka Simba yaibugiza Fountain Gate 4-0
Simba yaibugiza Fountain Gate 4-0
Read also
