Madrid, Hispania
Klabu ya Real Madrid ya Hispania Julai 16 itamtangaza rasmi mbele ya mashabiki 81,000 mshambuliaji wake mpya, Kylian Mbappe ambaye pia wametangaza kumpa jezi namba 9.
Mbappe amejiunga na klabu hiyo kwa mkataba wa miaka mitano akiwa mchezaji huru baada ya mkataba wake na klabu ya PSG ya Ufaransa kufikia ukomo Juni mwaka huu.
Utambulisho wa Mbappe unatarajia kuweka historia mpya ya klabu hiyo kwa kushuhudiwa na mashabiki wengi tangu klabu hiyo imtambulishe Cristiano Ronaldo mwaka 2009.
Utambulisho wa Mbappe unakuwa umehitimisha mbio za muda mrefu za Real Madrid kuisaka saini ya mchezaji huyo baada ya kujaribu katika vipindi viwili tofauti lakini kwa wakati wote kulikuwa na ugumu.
Bado haijawekwa wazi kama Mbappe atakuwa na klabu hiyo katika ziara za kujiandaa na msimu mpya wa 2024-25 nchini Marekani ambazo zitaanza hivi katibuni kwa timu hiyo kucheza mechi za kirafiki dhidi ya AC Milan, Barcelona na baadaye Chelsea.
Baada ya mechi hiyo, Real Madrid itacheza mechi ya Uefa Super Cup dhidi ya Atalanta, mechi itakayopigwa Agosti 14 na baada ya hapo Agosti 18, timu hiyo itaanza rasmi mbio za kulitetea taji la La Liga kwa kuuumana na Mallorca.
Mbappe alianza kuwindwa na Real Madrid tangu akiwa Monaco kabla ya kujiunga na PSG mwaka 2017 na hadi sasa ameifungia PSG mabao 256 katika misimu saba.
Kimataifa Mbappe kutambulishwa Madrid mbele ya mashabiki 81,000
Mbappe kutambulishwa Madrid mbele ya mashabiki 81,000
Read also
