Manchester, England
Klabu ya Manchester United injiandaa kuwafuta kazi wafanyakazi wake 250 ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kupunguza gharama pamoja na kupunguza baadhi ya shughuli za kiutendaji zisizo na ulazima.
Mkurugenzi wa klabu hiyo, Sir Dave Brailsford amefanya upembuzi wa kina wa shughuli za utendaji tangu Desemba mwaka jana baada ya kampuni ya Ineos kuthibitishwa kuwa mwekezaji mwenza wa klabu hiyo.
Awali mwenyekiti na mmiliki wa kampuni ya Ineos bilionea, Sir Jim Ratcliffe aliwahi kuwaambia wafanyakazi hao mapema kuhusu dhamira yake ya kuwataka waendelee kufanya kazi katika klabu hiyo.
Habari za ndani hata hivyo zinadai kwamba kwa sasa abadiliko makubwa ya kiuchumi yanahitaji kufanyika kwa lengo la kukabiliana na ongezeko la gharama mwaka hadi mwaka wakati mafanikio hayaonekani.
Uchambuzi na tathmini iliyofanywa na Sir Dave imebaini kwamba ukubwa na mfumo wa klabu haviendani na ubora wa soka la klabu hiyo ambayo imekuwa na maofisa watendaji wengi kuliko inavyohitajika.
Bado haijaweza kuwekwa wazi ni aina gani ya majukumu ambayo hayana ulazima lakini lengo ni kuhakikisha idadi ya watendaji inapungua pamoja na kupunguza gharama za waajiriwa wa klabu hiyo ambayo ina maofisa wapatao 1,150.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa muda wa klabu hiyo, Jean-Claude Blanc alitoa taarifa hiyo kwenye kikao cha wafanyakazi ambacho kilihudhuriwa na maofisa wa klabu hiyo wanaokadiriwa kufikia zaidi ya 800.
Kimataifa Wafanyakazi 250 kufutwa kazi Man United
Wafanyakazi 250 kufutwa kazi Man United
Read also
