Na mwandishi wetu
Aliyewahi kuwa mwenyekiti na mfadhili wa klabu ya Yanga, Yusuf Manji anatarajia kuzikwa leo Jumatatu huko Florida, Marekani.
Manji alifariki juzi Jumamosi akiwa hospitalini Florida na imeelezwa kuwa anazikwa katika jiji hilo kwenye makaburi aliyozikwa baba yake mzazi majira ya saa 9 alasiri eneo la Orlando, Florida.
Kwa mujibu wa taarifa ambayo imewekwa wazi na mtoto wa marehemu, Mehbub Manji imeeleza kuwa ingawa anazikwa Marekani lakini anatambua namna Watanzania walivyompenda na wanavyoendelea kumuombea mpaka sasa.
Manji alikuwa mwenyekiti wa Yanga kwa kipindi cha miaka mitano tangu mwaka 2012 hadi 2017 na kufanikiwa kusajili mastaa wakubwa wakiwemo Kelvin Yondani, Mbuyu Twite, Frank Domayo na Juma Kaseja.
Katika kipindi hicho Yanga chini ya Manji ilifanikiwa kutwaa makombe manne ya Ligi Kuu Bara, Kombe la FA, Ngao ya Jamii na Kombe la Kagame.
Soka Manji kuzikwa Marekani
Manji kuzikwa Marekani
Read also
