Na mwandishi wetu
Hatimaye ile habari ya kiungo Clatous Chota Chama au Triple C kuachana na klabu ya Simba na kujiunga na Yanga imetimia baada ya habari hiyo kuthibitishwa leo Jumatatu asubuhi.
Habari ya Chama kujiunga na Yanga imekuwa ikijadiliwa mitandaoni na kwenye vijiwe vya mashabiki kwa muda mrefu sasa lakini mapema leo picha za mchezaji huyo zimeonekana kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii akisaini kuichezea Yanga.
Picha iliyoonekana katika chanzo kimoja cha Yanga ilimuonesha mchezaji huyo akiwa anasaini na kuandamana na maneno yaliyosomea kwa herufi kubwa, ‘NYIE HAMUOGOPI?
Haikuweza kueleweka mara moja maneno hayo alikuwa akiambiwa nani au kundi gani lakini kwa uzoefu wa timu mahasimu za Simba na Yanga ni dhahiri swali hilo lina mtazamo wa kuwadhihaki Simba.
Habari ya Yanga kumsajili Chama inakuwa imemaliza majigambo na kozodoana kwa mashabiki wa timu hizo mbili mahasimu kwa kila mmoja kumpinga mwenzake kuhusu wapi angeelekea mchezaji huyo fundi wa kuuchezea mpira.
Katika taarifa ya Yanga hata hivyo haikuwekwa wazi mkataba wa mchezaji huyo ni wa muda gani na umeigharimu klabu hiyo kiasi gani cha fedha ingawa zipo habari kwamba Chama anakuwa mmoja wa wachezaji ghali katika klabu hiyo.
Soka Yametimia, Chama asaini Yanga
Yametimia, Chama asaini Yanga
Read also
