Na mwandishi wetu
Klabu ya Al Marreikh ya Sudan imemtangaza Murshid Ally Kika (pichani) raia wa Tanzania kuwa kocha wa viungo na utimamu wa mwili kwa wachezaji wa timu hiyo kuelekea msimu ujao wa 2024-25.
Murshid kabla ya kutua Marreikh aliwahi kuitumikia timu ya taifa ya Zanzibar chini ya Miaka 20 kwenye michuano ya Cecafa iliyofanyika Kenya na klabu ya Kundemba FC ya Zanzibar.
Kabla hajawa kocha aliwahi pia kucheza soka, timu ya taifa ya vijana U-17 (Serengeti Boys), pia ameitumikia klabu ya Azam na DTB ambayo baadaye ilikuja kuwa Singida Big Stars kisha Singida Fountain Gates na sasa Fountain Gates.
Al Marreikh ambayo ipo Tanzania ikijiandaa na mashindano mbalimbali yakiwemo ya Kagame yatakayofanyika Zanzibar na Dar es salaam pamoja na maandalizi ya kuelekea msimu ujao wa michuano mbalimbali watakayoshiriki.
Kwa Tanzania, imekuwa ni hatua kubwa kwa makocha wazawa ambao imekuwa nadra kupata nafasi ya kuzitumikia klabu za nje ya Tanzania hasa maeneo adimu kama hayo ya viungo na utimamu wa mwili wa wachezaji.
Soka Mtanzania kocha wa viungo Al Marreikh
Mtanzania kocha wa viungo Al Marreikh
Related posts
Read also
