Na mwandishi wetu
Kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kimeondoka leo Jumamosi kuelekea Ndola, Zambia kwa ajili ya mechi ya kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2026 dhidi ya Zambia.
Stars inakwenda kuivaa Zambia baada ya kujifua na mchezo wa kirafiki dhidi ya Indonesia ulioisha kwa suluhu na kisha kurejea Dar es Salaam na kufanya maandalizi ya mwisho kwa siku tatu.
Zambia itaingia katika mchezo huo utakaopigwa kuanzia saa 10 jioni kwenye Uwanja wa Levy Mwanawasa ikiwa na kumbukumbu ya kubugizwa mabao 2-1 na Morocco katika mchezo wa jana Ijumaa kwenye Uwanja wa Adrar mjini Agadir, Morocco.
Kaimu kocha mkuu wa Stars, Hemed Morocco ameeleza kufurahishwa na namna kikosi hicho kuwa tayari kwa ajili ya mtanange huo, wakionesha ari, kujiamini na kufahamu walichoelekezwa kwa ajili ya kutafuta pointi tatu muhimu ugenini.
Katika Kundi E, Morocco inaongoza kwa pointi sita, ikifuatiwa na Zambia, Niger na Tanzania zenye pointi tatu kila moja, Congo ni ya tano na Eritrea ya mwisho, zote zikiwa hazina pointi mpaka sasa.
Kimataifa Taifa Stars yaifuata Zambia
Taifa Stars yaifuata Zambia
Read also
