London, England
Mpango wa klabu za Ligi Kuu England (EPL) kupitia klabu ya Wolves wa kutaka matumizi ya teknolojia ya VAR yafutwe huenda ukakwama katika mkutano mkuu wa klabu za EPL Alhamisi hii.
Mapema mwezi uliopita Wolves waliwasilisha azimio katika mamlaka za EPL, azimio ambalo hata hivyo inadaiwa limeshawishi kuwapo kura za kutaka kuendelea na matumizi ya VAR au la.
Wolves wameendelea kusimamia msimamo wao wa kuliwasilisha suala hilo baada ya kukutana na maamuzi mengi mabaya dhidi yao katika mechi zao za msimu huu.
Azma hiyo ya Wolves hata hivyo huenda ikakwama kwani bado hakuna uhakika kama itaweza kupata kura 14 zinazohitajika ili azimio lao likubaliwe.
Habari zinadai kwamba baadhi ya klabu zinataka matumizi ya teknolojia ya VAR yaendelee kuwapo lakini hapo hapo klabu hizo zimesisitiza kuwapo maboresho katika teknolojia hiyo.
Klabu nyingine hata hivyo zinaamini matumizi ya VAR kwa wakati huu hayana faida na kuna mambo ya kuweka sawa katika jambo hilo.
Zipo habari kwamba klabu zenye nguvu katika EPL zinaamini mfumo wa VAR na mazingira ambayo yamekuwa yakijitokeza ni mambo ambayo yanaonyesha kuna tatizo ambalo linahitaji kuangaliwa kwa mapana.
Misimamo yote hiyo inatoa kila dalili za kuwapo hoja kinzani za kufuta au kutofuta matumizi ya VAR na uamuzi wowote utakaofikiwa utakuja baada ya kuwapo mjadala.
Mwamuzi mkongwe, Howard Webb ambaye pia ni kiongozi katika bodi ya waamuzi amewahi kusema kwamba mabadiliko katika VAR ni jambo ambalo linatakiwa kuangaliwa.
Kimataifa Kura kuikataa VAR kukwama?
Kura kuikataa VAR kukwama?
Read also
