Na mwandishi wetu
Fainali ya Kombe la Shirikisho la CRDB sasa itachezwa katika Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar badala ya Babati mkoani Manyara.
Hayo yamebainishwa leo Jumatano kupitia taarifa iliyotolewa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), ikielezwa kuwa uamuzi huo uliofanywa na Kamati ya Utendaji ya TFF umetokana na baadhi ya miundombinu muhimu mjini Babati kutokuwa tayari kwa ajili ya fainali hiyo pamoja na sababu za kiusalama.
Pamoja na kubadili uwanja wa fainali hiyo, TFF imezishauri mamlaka za mkoani Manyara kuendelea kufanya marekebisho katika miundombinu hiyo ili ifikiriwe kwa ajili ya fainali zijazo na michuano mingine mikubwa.
Fainali hiyo itakayozikutanisha Azam FC na Yanga SC inatarajiwa kuchezwa Juni 2, mwaka huu kuanzia saa 2.15 usiku ambapo TFF imemwalika Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wa Zanzibar, Mheshimiwa Tabia Maulid Mwita kuwa mgeni rasmi.
Soka Fainali Shirikisho kupigwa New Amaan
Fainali Shirikisho kupigwa New Amaan
Related posts
Read also
