Manchester, England
Kipa wa Man City, Ederson ataikosa mechi ya mwisho ya Ligi Kuu England (EPL) keshokutwa Jumapili pamoja na ile ya fainali ya Kombe la FA itakayopigwa Mei 25 baada ya kuumia jicho.
Mechi hizo mbili zimebeba hatma ya timu hiyo kubeba taji msimu huu, ukiacha ile ya FA dhidi ya Man United ambayo ni ya fainali, mechi ya EPL dhidi ya West Ham ndiyo itakayoamua hatma ya timu hiyo kama itabeba taji la EPL au la.
Jumanne iliyopita, Ederson, 30 alicheza mechi ya EPL dhidi ya Tottenham Hotspur ambayo walipata ushindi wa mabao 2-0 lakini alitolewa dakika ya 69 baada ya kugongana na Cristian Romero wa Spurs.
Man City inayoshika usukani EPL, Itaingia uwanjani kuikabili West Ham ikijua kuwa ni ushindi pekee utakaowahakikishia taji kwa mara ya nne mfululizo na baada ya hapo Mei 25 itaivaa Man United kwenye fainali ya Kombe la FA.
Mpinzani mkuu wa Man City katika kulisaka taji hilo ni Arsenal ambayo Jumapili hiyo hiyo nao watakuwa uwanjani kuumana na Everton, mechi ambayo pia wanatakiwa washinde ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kubeba taji la EPL msimu huu.
Kimataifa Ederson kuikosa fainali ya FA
Ederson kuikosa fainali ya FA
Read also
