London, England
Klabu ya Burnley hatimaye imeshuka daraja kutoka Ligi Kuu England (EPL) na sasa inarudi katika Ligi ya Championship ikiwa ni msimu mmoja tu baada ya kupanda EPL chini ya kocha Vincent Kompany (pichani).
Burnley imejikuta katika hali hiyo baada ya kushindwa kupata ushindi katika mechi yake dhidi ya Tottenham Jumamosi na kulala kwa mabao 2-1.
Kabla ya mechi hiyo hali ilikuwa wazi kwamba timu hiyo ilihitaji ushindi ili kuizidi Nottingham Forest iliyo nafasi ya nne kutoka mkiani kwani matokeo ya kufungwa au sare yasingeweza kuibeba timu hiyo ibaki EPL.
Ikiwa imebaki mechi moja kabla ya kumalizika kwa msimu wa 2023-24 wa EPL, Burnley ambayo si timu ngeni EPL, imezidiwa na Forest kwa tofauti ya pointi tano ambazo haiwezi kuzipata kwenye mechi moja iliyobaki.
Kitendo cha Burnley kushuka daraja kinaacha maswali kuhusu hatma ya Kompany, beki wa zamani wa Man City ambaye baada ya kuipandisha EPL ikiwa imetoka kubeba taji la Championship, matarajio yalionekana kuwa makubwa kutoka kwake.
Baada tu ya Burnley kupanda EPL, Kompany ambaye pia ni mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Ubelgiji, alisaini mkataba mpya na klabu hiyo na hadi sasa bado haijafahamika kama bodi itaamua kuendelea na kocha huyo au kuachana naye.
Kimataifa Burnely yashuka daraja
Burnely yashuka daraja
Read also
