Na mwandishi wetu
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) leo Jumanne limetangaza kikosi cha wachezaji 21 wa timu ya taifa, Taifa Stars kwa ajili ya mechi mbili za kirafiki zinazotarajiwa kupigwa wiki hii nchini Saudi Arabia.
Kikosi hicho chini ya kocha mkuu, Hemed Suleiman ‘Morocco’ (pichani) kilichosheheni vijana wengi na sura nyingi mpya kinatarajia kukwea pipa kesho Jumatano kuelekea Saudi Arabia kwa ajili ya mechi hizo mbili dhidi ya Sudan.
Wachezaji wanaounda kikosi hicho ni makipa; Ahmed Suleiman wa Uhamiaji, Abrahman Nassoro (Azam FC) na Ali Salim (Simba SC). Mabeki ni Mukrim Abdallah (Ihefu), Alphonce Mabula (RFK Novi Sad (Serbia), Miano Danilo (Alicante,Hispania), Gadiel Michael (Cape Town Spurs, Afrika Kusini), Abdulmalik Adam (Namungo), Baraka Mtuwi (Mashujaa) na Abdulrahim Bausi (Uhamiaji).
Viungo ni Mohammed Sagaf (Berham Wood, Uingereza), Morice Abraham (RFK Novi, Serbia), Khalid Habibu (Singida FG), Ishaka Mwinyi (KMC) na Jabir Seif (Getafe U-17, Hispania).
Safu ya ushambuliaji inaundwa na Omary Abdallah wa Mashujaa, Ben Starkie (Ilkeston Town, Uingereza), Oscar Adam (Kakamega FC, Kenya), Kelvin John (KRC Genk, Ubelgiji), Tarryn Allarakhia (Wealdstone, Uingereza) na Ibrahim Ahmada (Zimamoto FC).
Kuitwa kwa kikosi hicho chenye wachezaji wengi ambao ni ingizo jipya imeelezwa kuwa ni miongoni mwa mikakati kabambe ya kuelekea katika maandalizi ya michuano ya CHAN 2024 na ile ya Afcon 2027.
Soka Stars yenye sura mpya yatajwa
Stars yenye sura mpya yatajwa
Read also
