Na mwandishi wetu
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limeweka wazi droo ya robo fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho la CRDB kwa timu nane pekee zilizosalia katika mtanange huo.
Kwa mujibu wa TFF, Mechi za hatua hiyo zinatarajia kuanza kuunguruma, kati ya Mei 2 hadi Mei 4 mwaka huu.
Mabingwa watetezi wa kombe hilo, Yanga SC ambao walifika robo fainali kwa kuichapa Dodoma Jiji mabao 2-0 watamenyana na Tabora United iliyoichachafya Singida FG mabao 3-0.
Mashujaa ya Kigoma iliyoitupa Simba nje ya michuano hiyo kwa penalti 6-5, itaumana na Ihefu iliyoigonga KMC mabao 3-0 wakati Coastal Union ikiwa nyumbani itapepetana na Geita Gold na Azam FC itakuwa Azam Complex, Dar es Salaam ikiikaribisha Namungo.
Kwenye hatua ya nusu fainali inayotarajiwa kupigwa Mei 18 hadi 19, mwaka huu, mshindi kati ya Azam na Namungo atakutana na atakayepenya kati ya Coastal na Geita huku mshindi wa Ihefu na Mashujaa atacheza na atakayefuzu kati ya Yanga na Tabora.
Fainali ya michuano hiyo kwa msimu huu inatarajiwa kupigwa Juni 2, mwaka huu kwenye Uwanja wa Tanzanite, uliopo Babati Manyara.
Soka Droo Kombe la FA hadharani
Droo Kombe la FA hadharani
Read also
