Na mwandishi wetu
Klabu ya Azam FC imetangaza kumuongezea mkataba mpya wa miaka miwili beki wake wa kushoto, Pascal Msindo.
Azam imeeleza hayo leo Alhamisi kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii na kufafanua kuwa kulingana na umahiri wa beki huyo ambaye alijiunga na Azam akitokea akademi ya timu hiyo mwaka 2022 sasa atadumu hapo mpaka mwaka 2027.
“Mkataba umeongezwa, beki wetu mahiri wa kushoto, Pascal Msindo ataendelea kusalia kwenye viunga vya Azam hadi mwaka 2027 baada ya kuongeza mkataba mpya wa miaka miwili,” ilieleza taarifa hiyo.
Msindo ni miongoni mwa mabeki wanaochipukia vizuri na wanaoonekana msaada kwa timu hiyo katika kupigania ubingwa wa Ligi Kuu NBC msimu huu.
Kocha wa Azam, Youssuf Dabo aliwahi kukiri kuvutiwa na utendaji kazi wa kijana huyo ambaye makabrasha yake yanaonesha amezaliwa mwaka 2003.
Soka Msindo aongezewa mkataba Azam
Msindo aongezewa mkataba Azam
Read also
