Na mwandishi wetu
Mshambuliaji nyota wa kimataifa wa Tanzania, Clara Luvanga anayekipiga Al Nassr ya Saudi Arabia ameendeleza moto baada ya usiku wa kuamkia leo Alhamisi kufunga ‘hat-trick’ (mabao matatu).
Clara ambaye pia ni mchezaji wa timu ya wanawake ya Tanzania, alifunga mabao hayo kwenye ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya timu ya taifa ya Singapore katika mchezo wa kirafiki.
Nyota huyo wa zamani wa Yanga Princess amekuwa na muendelezo mzuri kwenye ligi ya nchini Saudia akifunga mabao 11 kwenye ligi hadi sasa na kuisaidia Nassr kuchukua ubingwa msimu huu.
Aidha, zimesalia mechi mbili kuamua hatma ya Mtanzania huyo kuchukua kiatu cha ufungaji bora akiwa kinara huku akifungana na Ibtissam Jraidi wa Al Ahli iliyopo nafasi ya pili kwenye msimamo.
Hata hivyo, Nassr imecheza mechi 12, ikipoteza mechi moja pekee na kushinda michezo 11, ikiwa imetwaa ubingwa wa nchi hiyo kwa pointi 31 ikiwa ni tofauti ya pointi 10 dhidi ya Al Ahli na Al Shabab zenye pointi 21 kila moja.
Kimataifa Clara apiga hat trick Saudi Arabia
Clara apiga hat trick Saudi Arabia
Read also
