Na mwandishi wetu
Nyota wa Yanga SC, Stephane Aziz Ki ametangazwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Machi akiwabwaga Feisal Salum ‘Fei Toto’ wa Azam na Clatous Chama wa Simba SC.
Aziz Ki raia wa Burkina Faso ametangazwa leo Jumanne na Kamati ya Tuzo za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) baada ya kuisaidia timu yake kupata ushindi katika mechi tatu kati ya nne ilizocheza katika mwezi huo.
Kwenye mechi hizo Aziz Ki alifunga mabao matatu na asisti nne na Yanga kuzoa pointi tisa ikisalia kwenye nafasi ya kwanza ya msimamo wa Ligi Kuu NBC.
Hii inakuwa mara ya pili msimu huu kwa Aziz Ki kuchukua tuzo ya mchezaji bora ambapo awali aliibeba mwezi Oktoba, mwaka jana.
Upande wa pili, kocha mkuu wa Azam FC, Bruno Ferry ametangazwa kuwa kocha bora wa mwezi Machi akiwashinda Miguel Gamondi wa Yanga na Zuberi Katwila wa Mtibwa Sugar alioingia nao fainali.
Kwenye mwezi huo Bruno aliiongoza Azam kushinda michezo miwili kati ya mitatu iliyocheza na kuendelea kusalia nafasi ya pili kwenye msimamo.
Bruno anatwaa tuzo hiyo kwa mara ya tatu msimu huu. Aliwahi kutwaa pia mwezi Novemba na Desemba, mwaka jana.
Soka Aziz Ki, Bruno wang’ara mwezi Machi
Aziz Ki, Bruno wang’ara mwezi Machi
Read also
