Na mwandishi wetu
Kocha mkuu wa timu ya taifa ya soka la watu wenye ulemavu ya Tanzania, Tembo Warriors, Salvatory Edward amesema kikosi chake kipo tayari kwa mashindano ya Mataifa ya Afrika (AAFCON) yatakayofanyika Misri kuanzia Aprili 14 hadi 29, mwaka huu.
Akizungumza na GreenSports, Edward (pichani) alisema kikosi chake kimeimarika na wanacheza kitimu hivyo ana imani watakwenda kuonesha ushindani kwenye mashindano hayo.
“Kikosi kipo imara na tangu tumekuja kambini Karatu tunafanya mazoezi asubuhi na jioni kwa sababu kila kitu kinapatikana hapa kambini, wachezaji wana ari na wanatamani muda wa mashindano ufike ili wakalipiganie taifa lao,” alisema Salvatory kiungo wa zamani wa Yanga.
Mashindano hayo yanashirikisha mataifa 16 ambayo yamepangwa katika makundi manne yenye timu nne kila moja na ndiyo yatakayoamua timu zitakazofuzu Kombe la Dunia la WAFF 2026.
Tanzania ambayo inashika nafasi ya saba kwa ubora duniani na ya nne Afrika itapambana na timu za Angola, Rwanda na Sierra Leone katika Kundi D wakati Kundi A linaundwa na Misri, Cameroon, Nigeria na Burundi.
Katika Kundi B kuna timu za Liberia, Morocco, Uganda na Senegal huku Kundi C likiwa na mataifa ya Ghana, Kenya, Gambia na Algeria.
Soka Tembo Warriors wapo tayari
Tembo Warriors wapo tayari
Related posts
Read also
