Paris, Ufaransa
Klabu ya PSG ya Ufaransa inadaiwa kutenga kitita cha Pauni 80 milioni kwa ajili ya kuinasa saini ya mshambuliaji wa Man United, Marcus Rashford ili achukue nafasi ya Kylian Mbappe.
Katika mpango huo, habari zaidi zinaarifu kuwa PSG pia ipo tayari kumlipa mshambuliaji huyo wa England mshahara wa Pauni 500,000 kwa wiki.
Hii si mara ya kwanza kwa PSG kuhusishwa na mipango ya kumsajili, Rashford, mwaka jana kigogo mmoja wa klabu hiyo alinukuliwa akisema kwamba, Rashford ni mmoja wa wachezaji ambaye wangependa ajiunge na timu hiyo.
Kinachoonekana kwa sasa ni kama vile PSG imeamua kuongeza nguvu katika mpango huo hasa kwa kuwa habari za Mbappe kuhamia Real Madrid zinazidi kupata nguvu siku hadi siku.
Tayari kocha wa PSG, Luis Enrique ameanza kulifanyia kazi suala zima la timu yake kucheza bila ya Mbappe kwa kuanza kumtupa benchi katika mechi kadhaa kwa anachodai kwamba mchezaji huyo ataondoka wakati wowote.
Kwa Rashford inatarajiwa atakuwa tayari kuikimbilia ofa ya PSG baada ya mambo yake kutokuwa mazuri msimu huu hadi kujikuta akitupiwa lawama na baadhi ya mashabiki kwenye mitandao ya kijamii wengi wao wakihoji uwajibikaji wake.
Rashford ambaye msimu uliopita alitamba kwa kuzifumania nyavu, alilazimika kuwajibu mashabiki hao waliohoji uwajibikaji wake na kuwataka wawe na ubinadamu katika jambo hilo.
Kimataifa Rashford aandaliwa pesa ndefu PSG
Rashford aandaliwa pesa ndefu PSG
Read also
