Paris, Ufaransa
Mshambuliaji wa timu ya PSG ya Ufaransa, Kylian Mbappe amemshitaki muuza kababu (mikate ya nyama) maarufu kwa kutumia mfano wa jina na muonekana wa mchezaji huyo ili kuipa hadhi moja ya mikate anayopika.
Muuza kababu huyo, Mohamed Henni ambaye ni maarufu na mwenye jina katika soka hasa nchini Ufaransa, amefungua duka la kuuza kababu katika jiji la Marseille.
Henni ambaye pia ni maarufu kwenye mitandao ya kijamii akiwa na wafuasi zaidi ya milioni moja katika Instagram tayari amefikishiwa taarifa za kushitakiwa huko jana Jumatano asubuhi.
Taarifa ya mawakili wa Mbappe ilimtaka Henni aondoe jina la Mbappe kwenye vyakula anavyouza kwa kipindi kisichozidi siku nane kabla ya kumfikisha mahakamani kwa kosa la kutumia jina la mchezaji huyo kibiashara bila ya ruhusa yake.
Uamuzi wa Mbappe ulimshutia Henni ambaye kwa kutumia mtandao wa Instagram alimjibu, ”Huoni hata aibu? Huna jambo jingine la kufanya? Unanishitaki kwa jambo lenye afya? Siamini.”
Mchezaji nyota wa zamani wa timu za Olympique Marseille na West Ham, Dimitri Payet ambaye kwa sasa anaichezea Vasco da Gama, naye jina lake limetumika katika moja ya mikate ya nyama kwa lengo la kukuza bishara.
Kimataifa Mbappe amshitaki muuza kababu
Mbappe amshitaki muuza kababu
Read also
