Paris, Ufaransa
Kocha wa PSG, Luis Enrique ameendelea kumuweka benchi Kylian Mbappe na kujikuta akipata sare ya mabao 2-2 dhidi ya Reims katika mechi ya Ligi 1 ikiwa ni sare ya tatu tangu aanze kumtupa benchi mshambuliaji huyo.
Enrique alifanya hivyo katika mechi mbili za awali za ligi hiyo hiyo kubwa nchini Ufaransa dhidi ya Rennes iliyoisha kwa sare pamoja na mechi dhidi ya Monaco ambayo pia iliisha kwa sare.
Katika mechi hizo mbili za awali, Mbappe alicheza kwa dakika 65 kila mechi na kutolewa lakini mechi ya juzi dhidi ya Reims, mshambuliaji huyo alianzia benchi kabla ya kuingia uwanjani dakika 20 mwisho.
Matokeo hayo hata hivyo yanaifanya PSG iendelee kushika usukani wa Ligi 1 pamoja na kuendeleza rekodi ya kutopoteza mechi hata moja kufikia mechi 20 licha ya kuwa ni sare ya tatu mfululizo.
Mbappe hadi sasa ana mabao 21 ya ligi na katikati ya wiki iliyopita alifunga mabao mwili katika ushindi wa 2-1 ambao timu hiyo iliupata katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Real Sociedad.
Uamuzi wa Enrique kumuweka mshambuliaji huyo benchi unatokana na kile alichodai kwamba PSG inatakiwa kuanza kufikiria maisha bila ya Mbappe ambaye yuko mbioni kuhamia Real Madrid baada ya msimu huu.
Kimataifa Mbappe aanzia benchi PSG ikipata sare ya tatu
Mbappe aanzia benchi PSG ikipata sare ya tatu
Read also
