Na mwandishi wetu
Simba imepata ushindi wa kupunguza presha katika Ligi Kuu NBC baada ya kuichapa Coastal Union mabao 2-1 ikiwa ni siku chache zimepita tangu ipokee kichapo kama hicho mbele ya Prisons.
Ushindi huo uliopatikana Jumamosi hii kwenye Uwanja wa CCM Mkwakwani mjini, Tanga unaifanya Simba kufikisha pointi 39 katika mechi 17 ingawa timu hiyo inabaki katika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi hiyo.
Simba ilianza kuzitingisha nyavu za Coastal Union katika dakika ya kwanza tu ya mchezo kwa bao lililofungwa na nyota wa timu hiyo kutoka Ivory Coast, Freddy Koublan.
Coastal Union walipambana na kufanikiwa kusawazisha bao hilo mfungaji akiwa kiungo wa timu hiyo, Lucas Almeida katika dakika ya 24 na kuzifanya timu hizo ziende mapumziko zikiwa sare ya bao 1-1.
Bao la ushindi lililoihakikikishia Simba pointi tatu muhimu za kwenye mechi hiyo lilipatikana katika dakika ya 73 mfungaji akiwa Willy Onana.
Matokeo hayo yanaifanya Coatal Union ibaki na pointi zake 27 katika mechi 20 ilizocheza hadi sasa na kujichimbia nafasi ya nne ikiwa pia imetanguliwa na Azam FC inayoshika nafasi ya pili na Yanga inayoshika usukani.
Soka Simba yaiadhibu Coastal 2-1
Simba yaiadhibu Coastal 2-1
Read also
