Na mwandishi wetu
Kocha mkuu wa Namungo, Mwinyi Zahera amesema siri ya ushindi wa bao 1-0 walioupata katika mechi yao na Kagera Sugar ni wachezaji wake kuanza kukifanyia kazi kile ambacho anawafundisha.
Huo ni ushindi wa kwanza kwa kocha huyo tangu akabidhiwe mikoba ya kuinoa timu hiyo mwanzoni mwa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu NBC.
“Tulikuwa bora kwenye maeneo mengi na ndicho ninachotaka wachezaji wangu wafanye na ushindi huu naamini utatuongezea ari ya kufanya vizuri mechi zijazo,” alisema Zahera.
Kwa upande wake kocha mkuu wa Kagera Sugar, Fredy Minziro alisema timu yake haikuwa na bahati katika mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Majaliwa, Lindi kwani walitengeneza nafasi nyingi lakini walishindwa kuzitumia.
“Nawapongeza Namungo kwa ushindi lakini pamoja na kupoteza mchezo tulikuwa bora kwa muda wote wa mchezo tunakubali matokeo na tunaangalia mechi inayofuata hivi sasa,” alisema Minziro.
Namungo ipo nafasi ya saba ikikusanya pointi 23 katika michezo 19 iliyocheza wakati Kagera inashika nafasi ya tisa kwa pointi 23 baada ya mechi 20 ilizoshuka dimbani.
Soka Zahera ataja siri ya ushindi Namungo
Zahera ataja siri ya ushindi Namungo
Read also
