Na mwandishi wetu
Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania, ‘Taifa Stars’, Miguel Gamondi amewaita katika kikosi chake wachezaji wawili wa timu ya vijana chini ya miaka 17 ya Tanzania maarufu Serengeti Boys.
Taarifa ya TFF iliyopatikana Ijumaa Mei 29, 2026 iliwataja wachezaji hao kuwa ni Kassim Juma na Luqman Mbalasalu ambao watajiunga katika kikosi hicho baada ya Juni 2, 2026.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo iliyosainiwa na ofisa habari na mawasiliano wa TFF, Cliford Ndimbo, Taifa Stars itacheza mechi ya kirafiki iliyopo kwenye kalenda ya Fifa dhidi ya Uganda Cranes, Ijumaa, Juni 5, 2026.
Baada ya mechi hiyo, Stars itaingia tena uwanjani Jumanne, Juni 9, 2026 kwa mechi yake ya pili dhidi ya timu ya Rwanda, mechi zote hizo zitachezwa mjini Marakech, Morocco.
Wachezaji wengine wa timu hiyo waliotajwa katika kikosi cha Gamondi, wameanza kuingia kambini tangu Ijumaa iliyopita.
Kwa upande wa Serengeti Boys, timu hiyo itacheza mechi ya fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) chini ya miaka 17 dhidi ya Senegal, mechi itakayochezwa mjini Rabat, Morocco, usiku wa Jumanne, Juni 2, 2026 kwenye Uwanja wa Moulay El Hassan.
Kimataifa Wawili Serengeti Boys waitwa Taifa Stars
Wawili Serengeti Boys waitwa Taifa Stars
Read also
