Rabat, Morocco
Timu ya soka ya Tanzania ya vijana chini ya miaka 17, Serengeti Boys, inasubiri kuikabili Senegal katika fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) kwa vijana chini ya miaka 17.
Serengeti imefikia hatua hiyo baada ya kuitoa Misri kwa mikwaju ya penalti 4-3 katika mechi ya nusu fainali baada ya sare ya bila kufungana.
Ushindi wa Serengeti Boys ni rekodi ya kujivunia kwa timu hiyo ambayo imefikia hatua hiyo kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania na sasa inasubiri kucheza mechi ya fainali usiku wa Jumanne, Juni 2, 2026 katika Uwanja wa Moulay El Hassan mjini Rabat.
Serengeti Boys ambayo iliingia katika michuano hiyo ikionesha kila dalili za kufika mbali, sasa ina kibarua kigumu dhidi ya Senegal moja ya timu zenye hadhi katika soka barani Afrika.
Mashabiki wa Serengeti Boys sasa wanasubiri kuiona timu yao ikiweka historia nyingine mpya na ya kipekee kwa kubeba taji la michuano hiyo.
Senegal wao wameweka heshima hadi kufikia hatua ya fainali wakiwa wamewatoa wenyeji Morocco mbele ya mashabiki wao jambo linalodhihirisha kwamba mechi yao na Serengeti itakuwa ngumu.
Ushindi wa Senegal dhidi ya Morocco ulianzia kwa bao la Mouhamed Wagne lakini wenyeji Morocco walipambana na kusawazisha kupitia kwa Ismail El Aoud na ndipo timu hizo zilipoingia kwenye mikwaju ya penalti na Senegal kushinda kwa penalti 7-6.
Morocco sasa itaumana na Misri katika mechi ya kusaka mshindi wa tatu ambayo itachezwa usiku wa Jumatatu, Juni 1, 2026.
Kimataifa Serengeti Boys vitani dhidi ya Senegal
Serengeti Boys vitani dhidi ya Senegal
Read also
